Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018 Ndg. Charles Francis Kabeho ameongoza mamia ya wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa katika sherehe za Mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa huku miradi minne ikizinduliwa na mmoja ukiwekewa jiwe la msingi.
Miradi hiyo ni pamoja na mradi wa maji kwa Afya ya Jamii Baura wenye uwezo wa kuhudumia wakazi 750 na maji yana uwezo wa kusambazwa
umbali usiozidi mita 200,mradi wa mabweni ya Wasichana Shule ya Sekondari Masawi yenye uwezo wa kulaza wanafunzi 128,mradi wa barabara ya Bereko-Munguri yenye umbali wa kilomita 15.6,mradi wa nyumba ya Walimu(Six in One) shule ya Sekondari Sakami yenye uwezo wa kuhudumia walimu sita.
Kiongozi huyo wa Mwenge amepongeza uongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kondoa kwa kusimamia vizuri miradi inayotekelezwa huku akikiri kuwani ya kiwango cha juu hivyo kuutendea haki Mwenge wa Uhuru.
Amepongeza pia jitihada za Halmashauri katika kuinua na kuboresha Elimu katika miundombinu na Taaluma,amesema jitihada hizo zinaendana na kauli mbiu ya Mbio za mwenge kwa mwaka 2018 inayosema "ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA WEKEZA SASA KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU".
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018,ndg. Charles Francis kabeho akizindua Barabara ya Bereko - Munguri yenye urefu wa kilomita 15.6
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018,ndg. Charles Francis kabeho akizindua Nyumba ya Walimu(Six in One) katika shule ya sekondari Sakami.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018,ndg. Charles Francis kabeho katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Kondoa Mhe. Sezaria Veneranda Makota(Wapili kushoto),Makamu mwenyekiti wa halmashauri Mhe. Hija Suru(Wa kwanza kushoto),Mkurugenzi wa Halmashuri ya Wilaya ya Kondoa Mwl.Falesy Mohamed Kibassa(wa tatu kushoto),Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Kondoa Ndg.Othman Gora(wa kwanza kulia) na Mratibu Elimu Kata kata ya Hondomairo Bw. Patrick Hando(aliyekaa)
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2018,ndg. Charles Francis kabeho akihutubia wananchi katika eneo lilioandaliwa kwa ajili ya mkesha wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 kata ya Hondomairo.
Baadhi wa wananchi waliohudhuria katika kilele cha Maadhimisho ya Mbio za Mwenge katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kata ya Hondomairo wakimsikiliza Kiongozi wa wa Mbio za Mwenge Akiongea.
KONDOA DISTRICT COUNCIL ,KILIMANI STREET
Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa
Simu : 0262360313
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.