Matokeo ya upimaji wa Kitaifa darasa la nne(SFNA),kidato cha pili(FTNA) 2019 na Mtihani wa Kidato cha nne(CSEE) na maarifa(QT) 2019 yametangazwa Rasmi leo tarehe 09 januari,2020.
Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde, ametangaza matokeo ya upimaji kitaifa darasa la nne, kidato cha pili na nne ya mitihani iliyofanyika Novemba 2019. Matokeo ya kidato cha nne mwaka 2019 yanaonyesha kuwa ufaulu umeongezeka kidogo kwa asilimia 1.4 kutoka ule wa mwaka 2018. Licha ya ufaulu huo kuongezeka, bado takriban nusu ama asilimia 48.6 ya watahiniwa wote wa mwaka 2019 wamepata daraja la nne.Necta imeeleza leo kuwa katika mtihani huo wanafunzi 340,914 wamefaulu mtihani kati ya wanafunzi 422,722 waliofanya mtihani huo Oktoba mwaka jana ikiwa ni sawa na asilimia 80.65 ya watahiniwa wote. Hii ni sawa na kusema kuwa wanafunzi 81 kati ya 100 waliofanya mtihani huo wamefaulu. Ufaulu huo, kwa mujibu wa Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde, ni sawa ongezeko la asilimia 1.38 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2018. Mwaka juzi asilimia 79.27 ya watahiniwa wa shule walifaulu mtihani huo.
Chagua kiunganishi unachotaka kisha Bofya.
1.MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE(CSEE) 2019 : https://matokeo.necta.go.tz/csee/csee.htm
2.MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA(QT)2019 : https://matokeo.necta.go.tz/qt/qt.html
3.MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2019 : https://matokeo.necta.go.tz/ftna/ftna.htm
4.MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2019 : https://matokeo.necta.go.tz/sfna5D/sfna.htm
KONDOA DISTRICT COUNCIL ,KILIMANI STREET
Anuani ya Posta: Box 1 Kondoa
Simu : 0262360313
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@kondoadc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa . Haki zote zimehifadhiwa.